Nyimbo Za Sifa
Wimbo 45 Ni Wako Wewe. Maneno ya wimbo
Ni wako Wewe, nikekujua
Na umeniamba
Lakini Bwana, nataka kwako
Nizidi kusongea
Chorus
Bwana vuta, vuta, nije
nisongee
Sana, kwako Mtini
Bwana vuta, vuta, nije
nisongee
Pa damu ya thamani
Niweke sasa nikatumike
Kwa nguvu za neema
Uyapendayo nami nipende
Nizidi kukwandama
Nina furaha tele kila saa
Nizungumzayo kwako
Nikuombapo nami napata
Kujua nia yako
Mapenzi yako hayapimiki
Ila ng’ambo ya liko
Anasa pia sitazijua
Bila kufika kwako