Nyimbo Za Sifa
Wimbo 2 Liko Lango Moja Wazi. Maneno ya wimbo
Liko lango moja wazi
Ni lango la Mbinguni
Na wote waingiao
Watapata nafasi
Longo ndiyeYesu Bwana
Wote waingie kwake
Lango! Lango
La Mbinguni ni wazi
Yesu ndiye lango hili
Hana sasa ni wazi
Kwa wakubwa na wadogo
Tajiri na maskini
Hili ni lango la raha
Ni lango Ia rehema
Kila mtu apitaye
Hana majonzi tena
Tukipita lango hili
Tutatoa mizigo
Tuliochukua kwanza
Tutavikwa uzima
Hima ndugu tuingie
Lango halijafungwa
Likifungwa mara moja
Halitafunguliwa