Nyimbo Za Sifa
Wimbo 184 Twaagana na Wapenzi. Maneno ya wimbo
Twaagana na wapenzi
Si “Kwa heri” lakini
Wampendao Mwokozi
Hao hawaachani
Watakuwako pamoja
Furahani, mbinguni
Furaha za kuonana
Kusema hatuwezi
Furaha hizi hatuna
Haziko siku hizi
TutamwonaYeye Bwana
Pamoja na wapenzi
Furaha za duniani
Kabisa zitakoma
Zisiingie moyoni
Nasi hatutasema
Furaha za kimbinguni
Huzidi kuwa njema
Basi hivi twaagana
Na wao kwa majonzi
Nasi twaamini sana
Tutamwona Mwokozi
Pamoja na wao, tena
Hao wafu wapenzi
Ewe Baba wa mbinguni
Twakushukuru sana
Kwa haya matumaini
Kuwa pamoja tena
Wapenzi wetu wa chini
Mbinguni kuwaona