Nyimbo Za Sifa
Wimbo 17 Ndiyo Dhamana,Yesu Wangu. Maneno ya wimbo
Ndiyo dhamana,Yesu wangu
Hunipa furaha za Mbingu
Mrithi wa wokovu wake
Nimezawa Kwa Roho yake
Chorus
Habari njema, raha yangu
Yesu ndiye Mwokozi wangu
Habari njema, raha yangu
Yesu ndiye Mwokozi wangu
Kumsalimu moyo wangu
Mara namwona raha yangu
Aniletea malaika
Wananilinda, taokoka..
Sina kinyume, nashukuru
Mchana kutwa huja kwangu
Usiku kucha kuna nuru
Mwokozi wangu; ndimi huru
Hall na mali, anitwaa!
Mara namwona anifaa
Nami nangoja kwa subira
Akiniita, nije mara