Nyimbo Za Sifa
Wimbo 16 AkifaYesu Nikafa Naye. Maneno ya wimbo
Akifa Yesu nikafa naye
Uzima upya hushi naye
Humtazama mpaka aje
Nyakati zote ni wako Yeye
Chorus
‘Nyakati zote nimo pendoni
Nyakati zote ni uzimani
Humtozama hata atokee
Nyakati zote mimi ni wake
Vita sipigi visivyo haki
Na Bwana wangu hapiganiki
Beramu yake haitwaliki
Napo po pote hiia sitaki
Sina mashaka, akawa mbali
Mizigo yote aihimili
Ananituliza lmanweli
Nyakati zote mimi husali
Sina huzuni na mimi sidhii
Simwagi chozi, wala siguni
Sikuti afa, Ila Kitini
Daima hunifikiri mimi
Kila unyonge huusikia
Kila ugonjwa kwake hupoa
Yesu ni mwenye kuniokoa
Nyakari zote hunijalia.