Nyimbo Za Sifa
Wimbo 141 Waimba, Sikizeni. Maneno ya wimbo
Waimba, sikizeni,
Malaika Mbinguni;
wimbo wa tamu sana
Wa pendo zake Bwana;
“Duniani salama,
Kwa wakosa rehema.”
Sisi sote na twimbe
Nao wale wajumbe;
Waimba, sikizeni,
Malaika Mbinguni.
Ndiye Bwana wa Mbingu,
Tangu milele Mungu.
Amezaliwa mwili,
Mwana wa mwanamwali;
Ametoka enzini
Kuja ulimwenguni
Mwokozi atufie,
Ili tusipotee.
Waimba, sikizeni,
Malaika Mbinguni.
Mtukufu wa amani
Ametoka Mbinguni,
Jua Ia haki, ndiye
Atumulikiaye;
Amejivua enzi,
Alivyo na mapenzi,
Ataka kutuponya,
Kutuzalisha upya,
Waimba sikizeni,
Malaika Mbinguni.
Njoo upesi, Bwana,
Twakutamani sana;
Kaa nasi, Mwokozi
Vita hatuviwezi;
Vunja kichwa cha nyoka,
Sura zako andika,
Tufanane na Wewe,
Kwetu sifa upewe,
Waimba, sikizeni,
Malaika Mbinguni.