Nyimbo Za Sifa
Wimbo 132 Leo Mwana Amezaliwa. Maneno ya wimbo
Leo Mwana amezawa
Kwa ajili yetu
Ndiye atakayekuwa
Mtawala wetu
Leo siku yake kuu
Msifuni Mungu
jina lake ndilo hili
Bwana wa Salama
Ameitwa lmanweli
Ni Mwenye uzima
Leo siku yake kuu
Msifuni Mungu
Ndiye Mtawala bora
Hapungui nguvu
Milki yake ni imara
Na utimilivu
Leo siku yake kuu
Msifuni Mungu
Jesu ndiye huyo Mwana
Bwana wa salama
Mwenye enzi bora sana
Na Mwenye hekima
Leo siku yake kuu
Msifuni Mungu
Leo alikuja kwetu
Hata kwa dunia
lli aokoe watu
Kwa kuwafilia
Leo siku yake kuu
Msifuni Mungu