Nyimbo Za Sifa
Wimbo 10 Nina Haja Nawe. Maneno ya wimbo
Nina haja nawe
Kila saa;
Hawezi mwingine
Kunifaa.
Chorus
Yesu, nakuhitaji
Vivyo kila saa!
Niwezeshe, Mwokozi
Nakujia.
Nina haja nawe;
Kaa nami,
Na maonjo haya,
Hayaumi.
Nina haja nawe;
Kila hali,
Maisha ni bure’
Uli mbali.
Nina haja nawe,
Nifundishe
Na ahadi zako
Zifikishe.
Nina haja nawé
Mweza yote,
Ni wako kabisa
Siku zote.