Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 99 TWENDE KWA YESU nyimbo za wokovu
1
Twende kwa Yesu mimi nawe,
njia atuonya tuijue,
Imo Chuoni; na mwenyewe,
hapa asema njoo!
Na Furaha tutaiona,
mioyo ikitakata sana;
Kwako, Mwokozi, kuonana,
na milele kukaa.
2
Wana na aje, atwambia
furahini kwa kusikia
Ndiye Mwokozi wetu hasa,
na tumtii, njoni.
3
Wangojeani? Leo yupo:
sikiza sana asemapo;
Huruma zake zitwitapo,
ewe kijana, njoo.