Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 97 SIOSHWI DHAMBI ZANGU? nyimbo za wokovu
1
Sioshwi dhambi zangu?
Bila damu yake Yesu,
Hapendezewi Mungu
bila damu yake Yesu.
Hakuna kabisa
Dawa ya makosa
Ya Kututakasa
Ila Damu yake Yesu.
2
La kunisafi sina,
Ila damu lake Yesu.
Wala udhuru tena,
Ila damu yake Yesu.
3
Sipati patanishwa,
Bila damu yake Yesu,
Hukumu yanitisha,
Bila damu yake Yesu.
4
Sipati tumaini
Bila damu yake Yesu,
Wema wala amani
Bila damu yake Yesu.
5
Yashinda ulimwengu,
Iyo, damu yake Yesu,
Na kutufikisha juu,
Iyo, damu yake Yesu.