Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 88 SIKU HII YA SABATO nyimbo za wokovu
1
Siku hii ya Sabato,
Tamu kufikiri
Juu ya Mungu na Mbingu
Kuacha dunia.
2
Tamu kusikia Neno
Toka mhubiri
Anayefundisha toba,
Tupate uzima.
3
Katika vita na dhambi,
Ikiwa twashindwa,
Yeye atutupa nguvu
Aonaye moyo.