Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 77 HABARI ZA USIKU nyimbo za wokovu
1.Je! Mlinzi ukutani
Wa mji wa Zayuni,
Habari zake usiku?
Asubuhi karibu?
Kuna dalili za kupambazuka?
Kuna dalili za kupambazuka?
2
Katika safari yetu
Twaona nchi kavu?
Tutalala baharini?
Bandari bado mbali?
Kweli, kweli tutaona ufalme?
Kweli, kweli tutaona ufalme?
3
Tunaona nuru yake
Nyota ya asubuhi;
Nyota, tukufu na safi.
Inang’aa mbinguni;
Furahini, wokovu u karibu.
Furahini, wokovu u karibu.
4
Tumetazama ramani.
Kweli pwani si mbali;
Twende mbele, kwa upesi.
Tutaona bandari;
Furahini, imbeni nyimbo zenu.
Furahini, imbeni nyimbo zenu.