Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 73 BWANA, UNIONGOZE JUU nyimbo za wokovu
1
Nakaza mwendo mbinguni,
Kila siku napanda juu;
Naomba nikisafiri,
Bwana uniongoze juu
Bwana uniinue juu
kwa imani hata mbingu.
Juu kuliko dunia;
Bwana uniongoze juu.
2
Moyo wangu hautaki
kukaa palipo shaka;
Wengine wapenda chini
Nia yangu ni kupanda.
3
Nataka kupanda juu
Nisishindwe na adui;
Kwa imani nasikia
Sauti ya washindaji.
4
Kupanda juu nataka
Niuone utukufu;
Hata mwisho nitaomba,
Bwana uniongoze juu