Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 68 TUSIMAME IMARA MWAMBANI nyimbo za wokovu
1
Umtetee Mungu duniani
ijapo pepo kali zavuma;
Mwambani pekee pana nguvu
dhambi ikilemea.
Tusimame imara katika mwamba,
Mwamba wa Kristo pekee;
Ndipo salamini tutasimama
Kule kitini pa enzi.
2
Itetee haki kwa bidii,
kwa moyo mnyofu wa imani;
Mwambani pekee utashindwa
wingi wa upotovu.
3
Itetee kweli, itadumu,
ijapokawia itashinda;
Mwambani pekee pana raha
yaishapo tufani.