Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 64 PIGA PANDA YA INJILI nyimbo za wokovu
1
Piga panda ya Injili,
Onyesha watu wote:
Ili anayesikia
Atubu, aokoke.
Piga panda ya Injili,
uipige kwa nguvu:
Mungu amekuagiza
mateka wawe huru.
2
Uipige vilimani,
kwa kila tambarare:
Pande zote, miji yote
isikie Injili.
3
Uipige mipakani,
barabarani pia;
Iwatangazie wote,
wanakwita na Baba.
4
Uipige! Watu wengi
wataka wawe huru;
Waambie kwamba
Yesu asema ‘Njoni kwangu’