Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 59 FANYENI KAZI ZENU nyimbo za wokovu
1
Fanyeni kazi zenu,
Usiku si mbali;
Kesheni saa zenu
Vumilieni;
Kwa Yesu tumikeni
Na hio Injili.
Sana wahubirini
Watu wa mbali.
2
Fanyeni kazi zenu
Giza yasongea;
Na wengi wenzi wenu
wamo gizani.
Msipoteze moja
Dakika ni hizi:
Bwana atarejea
Mwisho wa kazi.
3
Fanyeni kazi zenu,
Hivi jua lachwa;
Wote walio kwenu
Apenda Mungu:
Na sisi tumjuaye
Na tuwafundishe
Ili Yesu ajaye
Tumfurahishe.