Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 56 WAPONYENI WATU nyimbo za wokovu

Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns

Wimbo 56 WAPONYENI WATU nyimbo za wokovu

 

1
Walio kifoni, nenda waponye,
Uwatoe walio shimoni;
Wanaoanguka uwainue;
Habari njema uwajulishe.

Walio kifoni waokoeni,
Mwokozi yuko huwangojea.

2
Wajapokawia anangojea,
Awasubiri waje tobani;
Mwokozi hawezi kuwadharau,
Huwasamehe tangu zamani;

3
Na ndani ya moyo wa wanadamu
Huwamo shida, tena huzuni;
Lakini kwa Yesu kuna rehema
Kuwaponya na kuwaokoa.

4
Walio kifoni, nenda waponye
Kazi ni yetu, zawadi iko;
Nguvu kuhubiri Bwana hutoa
Kwa subira tuwavute sasa

Exit mobile version