Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 49 NINAYE RAFIKI nyimbo za wokovu
1
Ninaye Rafiki naye
Alinipenda mbele;
Kwa kamba za pendo lake
Nimefungwa milele;
Aukaza moyo wangu,
Uache ugeuzi,
Ninakaa ndani yake,
Yeye kwangu, milele.
2
Ninaye Rafiki ndiye
Aliyenifilia;
Alimwaga damu yake
Kwa watu wote pia;
Sina kitu mimi tena,
Nikiwa navyo tele;
Pia vyote ni amana
Ndimi wake milele.
3
Ninaye Rafiki naye
Uwezo amepewa,
Atanilinda mwenyewe,
Juu ‘tanyakuliwa;
Nikitazama mbinguni
Hupata nguvu tele;
Sasa natumika chini,
Kisha juu milele.
4
Ninaye Rafiki naye
Yuna na moyo mwema,
Ni Mwalimu, Kiongozi,
Mlinzi wa daima;
Ni nani wa kunitenga
Na mpenzi wa mbele?
Kwake nimetia nanga,
Ndimi wake milele.