Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 47 NI HERI KIFUNGO nyimbo za wokovu
1
Ni heri kifungo
Kinachotufunga
Mioyo yetu kwa pendo
Pendo la Kikristo
2
M-bele ya Baba
Tunatoa sala;
Hofu, nia, masumbufu
Yetu ni mamoja.
3
Tunavishiriki
Matata na shida,
Na mara nyingi twatoa
Chozi la fanaka
4
Tunapoachana
Moyoni twalia;
Lakini tutakutana
Mwisho juu mbinguni.