Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 42 EWE ROHO WA MBIGUNI nyimbo za wokovu
1
Ewe Roho wa mbinguni,
Maombi sikia!
Makao yako yafanye
Mioyoni mwetu.
2
Kama nuru, tupenyeze,
Giza uondoe;
Siri yako tuione,
Na amani yako.
3
Kama moto, tusafishe,
Choma dhambi yetu;
Roho zetu ziwe zote
Hekalu la Bwana.
4
Kama umande, na uje,
Utuburudishe,
Moyo kavu utakuwa
Ni wenye Baraka.
5
Kama upepo Ee Roho,
Katika Pentekoste
Ukombozi utangaze,
Kwa kila taifa.