Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 34 HADITHIA KISA CHA YESU nyimbo za wokovu
1
Nipe Habari za Yesu,
Kwangu ni tamu sana
Kisa chake cha thamani
Hunipendeza sana.
Jinsi malaika wengi
walivyoimba sifa.
Alipoleta amani
Kwa watu wa dunia.
Nipe habari za Yesu,
Kaza moyoni mwangu;
Kisa chake cha thamani
Hunipendeza sana.
2
Kisa cha alivyofunga
peke yake jangwani.
Jinsi alivyolishinda
Jaribu la Shetani;
Kazi aliyoifanya,
Na siku za huzuni,
Jinsi walivyomtesa:
Yote ni ya ajabu!
3
Habari za Msalaba
Aliposulubishwa:
Jinsi walivyomzika
Akashinda kaburi.
Kisa chake cha rehema.
Upendo wake kwangu,
Aliyetoa maisha
Nipokee wokovu.