Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 23 YESU FURAHA YA MOYO nyimbo za wokovu
1
Yesu, furaha ya moyo!
Hazina ya pendo, na nuru.
Yote yatupendezayo,
Yasilinganishwe nawe.
2
Kweli yako ya daima,
Wawajibu wakwitao,
Ni siku zote u mwema
Kwao wakutafutao.
3
U Mkate wa Uzima,
Kupokea ni baraka,
Twanywa kwako u kisima
Roho zikiburudika.
4
Mwokozi twakutamani,
Kwako roho hutulia
Twakushika kwa imani,
Nawe watubarikia.
5
Yesu, ndiwe kwetu mwanga,
Tufurahishe daima
Giza ya dhambi fukuza,
Uwe mwanga wa Uzima.