Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 201 HUNIPENDA PIA nyimbo za wokovu
1
Mungu huona videge
Wanaoanguka;
Akawapenda videge,
Vile hunipenda.
Hunipenda, hunipenda,
Hunipenda pia;
Najua ananipenda
Niliye mdogo.
2
Rangi ya namna nzuri
Hupamba maua;
Akiyapenda maua,
Vile hunipenda.
3
Mungu aliyeviumba
Videge, maua,
Hatasahau watoto,
Kweli huwapenda.