Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 197 ANIPENDA NI KWELI nyimbo za wokovu
1
Anipenda ni kweli:
Mungu anena hili:
Sisi wake watoto
Kutulinda si zito.
Yesu Mwokozi
ananipenda:
Kweli hupenda.
Mungu amesema.
2
Kwa kupenda akafa
Niokoke na kufa:
Atazisafi taka
Sana ataniweka.
3
Anipenda kabisa;
Niuguapo sasa.
Anitunza mbinguni
Niliyelala chini.
4
Kunipenda haachi
Tu sote hapa chini,
Baada ya mashaka
Kwake tanipeleka.