Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 187 KUFARIKI NAYE YESU nyimbo za wokovu
1
Kufariki naye Yesu!
Usingizi wenye heri:
Raha isiyofujika
Kwa majonzi na adui
2
Kufariki naye Yesu!
Lo! ya kubwaga simanzi
Na kulala na amani
Hata Bwana awatuze.
3
Kufariki naye Yesu!
Heri watakaoamshwa.
Wataona siku ile
Utukufu wake Bwana.
4
Kufariki naye Yesu!
Wataamka aitapo:
Watapasua kaburi
Na kutoka watukufu.