Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 182 HAPANA GIZA nyimbo za wokovu
1
Mchana hauishi
Mjini mzuri;
Mji hautapita;
Na hapana giza.
Machozi yatafutwa,
Kifo hapana pale
Hawahesabu siku,
Na hapana giza
2
Milango ni ya lulu,
Mjini mzuri;
Dhahabu njia zake;
Na hapana giza.
3
Mlango haifungwi
Mjini mzuri;
Mto ni wa uzima
Na hapana giza.
4
Hawahitaji jua
Mjini mzuri,
Mwana Kondoo nuru;
Na hapana giza.