Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 177 KAZI YANGU IKISHA nyimbo za wokovu
1
Kazi yangu ikisha,
Nami, nikiokoka,
Na kuvaa kutokuharibika.
Nitamjua Mwokozi;
Nivukapo ng’amboni
Atakuwa wa kwanza
Kunilaki.
Nitamjua, nitamjua,
Nikimwona uso kwa uso;
Nitamjua, nitamjua
Kwa alama za misumari.
2
Kuona uso wake
Kutanipa furaha,
Furaha isiyo ya kukomesha;
Nitamsifu Mwokozi
Kwa rehema na pendo.
Vilivyonipa pahali
Mbinguni.
3
Nao waliokufa
Katika Bwana Yesu,
Nitawaona tena huko juu;
Lakini nifikapo kwake
Huko mbinguni,
Nataka kumwona
Mwokozi kwanza.
4
Milangoni mwa mji
Bwana atanipisha,
Pasipo machozi
Wala huzuni.
Nitauimba wimbo
Wa milele; Lakini
Nataka kumwona
Mwokozi kwanza.