Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 176 ATI TUONANE MTONI? nyimbo za wokovu
1
Ati twonane mtoni?
Maji mazuri ya mbingu
Yanatokea mwangani,
Penye kiti cha Mungu.
Naam, twonane mtoni!
Watakatifu, kwenu ni mtoni!
Tutakutanika kule mtoni
Penye kiti cha Mungu.
2
Tukitembea mtoni
Na Yesu Mchunga wetu
Daima tu ibadani
usoni pake kwetu.
3
Tukisafiri mtoni
tutue ulemeao
Wema wa Mungu yakini:
una taji na vao!
4
Kwangara sana mtoni
cha Mwokozi ni kioo
Milele hatuachani
Tumsifu kwa nyimbo.
5
Karibu sana mtoni,
Karibu tutawasili
Mara huwa furahani
na amani ya kweli.