Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 173 HATUJUI SAA nyimbo za wokovu
1
Hatujui sa-a
Ya kuja kwa Bwana,
Lakini dalili
Zasema karibu
Atakaporudi,
Lakini kwa kweli
Hatujui sa-a.
Atakuja,
Kwa vile tukeshe;
Atakuja
Mwokozi, Aleluya!
Atakuja kwa fahari
Ya Baba yake,
Hatujui saa.
2
Pana nuru kwao
Wapendao haki,
Pana kweli katika
Chuo cha Mungu;
Unabii hufundisha
Kuja kwake,–
Hatujui saa.
3
Tutakesha na
Tutaomba daima,
Tutafanya kazi
Mpaka akija,
Tutaimba na
Tutasoma ishara,-
Hatujui saa.