Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 17 SI MIMI, KRISTO nyimbo za wokovu
1
Si mimi, Kristo
Astahili sifa;
Si mimi, Kristo
Ajulikane;
Si mimi, Kristo
Katika maneno
Si mimi, Kristo
Kwa kila tendo
2
Si mimi, Kristo,
Kuponya huzuni;
Kristo pekee,
Kufuta machozi;
Si mimi, Kristo,
Kubeba mzigo;
Si mimi, Kristo,
Kupunga hofu
3
Kristo Pekee,
Pasipo kujisifu
Kristo pekee,
Na nisizungumze
Kristo pekee,
Na hakuna kiburi
Kristo pekee,
Sifa yangu ife
4
Kristo pekee,
Mahitaji atoe
Si mimi, Kristo,
Kisima changu.
Kristo pekee,
Kwa mwili
Na kwa moyo
Si mimi, Kristo,
Hata milele