Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 163 ANAKUJA BWANA YESU nyimbo za wokovu
1
Pengine ni saa
Ya kupambazuka,
Mishale ya jua
Ipenyapo giza,
Kwamba atakuja
Yesu mtukufu,
Awapokee wake.
Bwana itakuwa
Lini Tutakapoimba,
Anakuja, Bwana Yesu,
Aleluya, Amin,
Aleluya, Amin?
2
Pengine mchana,
Pengine usiku
Wa manane, giza
Itatoweka
Kwa fahari akija,
awapokee wake.
3
Majeshi yake
Yataimba ‘hosana,’
Na watakatifu
Waliotukuzwa
Watamsifu
Kwa kuwa amekuja
Awapokee wake.
4
Furaha tukiitwa
Pasipo kufa,
Pasipo kuona
Maradhi, machozi;
Kuchukuliwa
Winguni kwa fahari
Akija kwa watu wake.