Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 16 BWANA NINAKUHITAJI nyimbo za wokovu
1
Bwana ninakuhitaji!
Ni mpofu, maskini;
Unishike mkononi,
Kwako Napata nguvu.
Kila saa, Kila saa
Bwana ninakuhitaji;
Kila saa, Kila saa,
Unilinde Kila saa.
2
Univike na mavazi
Ya usikivu wako;
Nguo zangu ni machafu,
Nazitamani zako.
3
Wewe ukiniongoza
Nitakwenda salama;
Nenda nami siku zote,
U nuru na uzima.
4
Na ikiwa m-beleni
Sehemu yangu ngumu,
Au ikiwa furaha,
Unilinde kila saa.