Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 159 ANAKUJA UPESI nyimbo za wokovu
1
Anakuja upesi,
Yesu Bwana wetu,
Msafiri mbali na kwao;
Alisema dhahiri,
Nitakuja tena
Amina na uje,
E Bwana.
Yuaja,
Yesu atarudi sasa;
Anakuja duniani.
Wasafiri wote
Watapumzika
Yesu anaporudi tena.
2
Makaburi yote
Wafu wanapolala
Yatafunguliwa tena;
Na mamilioni pale
Wataondoka tena,
Wasione machozi kamwe.
3
Aleluya Amin!
Aleluya tena!
Upendo wake unashinda,
Tutamsifu milele,
Hata tutashangaa,
Jinsi alivyotukomboa.