Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 150 HASHA, MANENO MABAYA YASITOKE nyimbo za wokovu
1
Hasha, maneno mabaya
Yasitoke kinywani
Moyo mwema uzuie
Ndimi, zisichafuke.
Nanyi pendeni
Asema Yesu,
(mpendane) (mpendane)
Kama mwanzo alivyotupenda:
Nanyi pendeni
Asema Yesu,
(mpendane) (mpendane)
Wana, tiini amri hii,
(amri heri hii).
2
Pendo ni mtakatifu,
Urafiki; mzuri:
Visiharibike mara
Kwa kunena vibaya
3
Tusinene kwa hasira,
Inazaa huzuni.
Pendo lako, ee Mwokozi,
inatosha tushinde.