Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 149 KUWA WAKE YESU nyimbo za wokovu
1
Kuwa wake Yesu,
Je! ni kusudi lako?
Ungeenda naye
Njia nyembamba?
Unataka aubebe
Mzigo wako?
Awe Mwongozi wako.
Uwezo wake
Unakutosha;
Na damu yake
Itakusafi;
Kwa vile ukubali
Ni bora;
Afanye mapenzi
Yake nawe.
2
Unataka kuitika
Anapokwita?
Kupata amani
Kwa kumpa vyote?
Wataka uwezo
Usianguke kamwe?
Awe Mwongozi wako.
3
Wataka raha
Katika ufalme wake?
Ungeshinda kwa
Majaribu yote?
Ungefanya kazi
Yake vizuri sana?
Awe Mwongozi wako.