Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 13 YESU UJE KWETU nyimbo za wokovu
1
Umetuahidi kwamba wawili
Watatu, kwa jina lako wakija,
Utawabariki; kwa hivi leo
Twapiga magoti nyumbani pako.
Yesu uje kwetu Utubariki;
Yesu uje kwetu Uwe Karibu.
2
Umekuwa nasi siku nyingine
Tunakuhitaji mpaka mwisho.
Uje Mwokozi, tupe neema;
Tusikie Yesu, utubariki.
3
Uje utawale sauti zetu:
Nyimbo, nazo sala uziagize.
Imani izidi, ikamilike;
Pendo liwe safi, na njia nuru.