Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 120 MSALABA WA YESU nyimbo za wokovu
1
Msalaba wa Yesu,
Nikae karibu;
Pale pana chemchemi
Ya kuponya dhambi.
Pale msalaba
Msalaba wake,
Huo ni sifa yangu
Kwa maisha yote.
2
Karibu msalaba
Nalitetemeka,
Pendo likaniona
Likanirehemu.
3
Unikumbushe, Yesu,
Nikuone pale;
Niupate upendo
Na kuvutwa nao.
4
Karibu msalaba,
Kwa kutegemea,
Kukesha na kungoja,
Nitakaa pale.