Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 118 NILIPOTOKA KABISA nyimbo za wokovu
1
Nilipotoka kabisa,
Sasa narudi;
Nikakawia dhambini,
Bwana narudi.
Narudi nyumbani;
Daima kwako.
Kwa upendo nipokee:
Naja nyumbani.
2
Nikasusurika sana,
Sasa narudi;
Mwenye uchungu natubu,
Bwana narudi.
3
Nimechoka maovuni,
Sasa narudi;
Pendo lako lanivuta,
Bwana narudi.
4
Ndilo tumaini langu,
Sasa narudi;
Yesu alinifilia,
Bwana narudi.
5
Damu yake yanitosha,
Sasa narudi;
Unioshe kenyekenye,
Bwana narudi.