Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 114 YESU NATAKA KUTAKASWA SANA nyimbo za wokovu

Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns

Wimbo 114 YESU NATAKA KUTAKASWA SANA nyimbo za wokovu

 

1
Yesu Mwokozi ili nitakaswe,
Nataka moyo uwe enzi yako.
Ukiangushe kilichoinuka
unioshe sasa niwe mweupe.

Mweupe tu, ndiyo mweupe,
Ukiniosha nitakuwa safi.

2
Bwana Yesu sasa unitazame,
unifanye niwe dhabihu hai.
Najitoa kwako, na moyo, vyote;
unioshe sana niwe mweupe.

3
Bwana kwa hivyo nakuomba sana,
nakungojea miguuni pako
Wanaokuja hutupi kamwe,
unioshe sasa niwe mweupe.

Exit mobile version