Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 110 MLANGO WAZI nyimbo za wokovu
1
Mlango uko wa wema,
Mlango wazi huo
Yesu ameufungua
Na hakuna kufunga.
Mlango wazi, ajabu,
Uliachwa wazi kwangu?
Kwangu, kwangu?
Wazi, wazi kwangu?
2
Mlango hukaa wazi
Watu waokolewe;
Maskini na matarajiri
Wa mataifa yote.
3
Maadam mlango wazi
Rafiki kaza mwendo;
Msalaba ukubali
Amana ya upendo.
4
Msalaba tutabeba
Daima, na furaha
‘Pendo wa Yesu hushinda,
Tunainama kwake