Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 102 MLANGONI PA MOYO nyimbo za wokovu
1
Mlangoni pa moyo;
Mgeni! (Amesimama)
Amesimama pale,
Mgeni! (Amesimama)
Umkaribishe sasa,
Umkaribishe Mwana
Wa Baba wa upendo:
Mgeni! (Umkaribishe)
2
Moyo wako kwa Bwana
Fungua. (Fungulieni)
Asikuache mbali,
Fungua. (Fungulieni)
Umkubali Rafiki,
Roho atafariji
Naye atakutunza:
Fungua. (Fungulieni)
3
Usikie sauti
Ya Bwana. (Uisikie)
Uyachague mambo
Ya Bwana, (Mambo ya Bwana)
Ufungue mlango,
Usimwambie bado:
Jina lake tumai
Yu Bwana. (Jina la Bwana)
4
Na ufungue moyo,
Kwa Bwana (Fungulieni)
Utapewa msaada,
Wa Bwana (Msaada wetu)
Uzuri Utavikwa,
Dhambi ataondoa,
Ukifungua moyo.
Kwa Bwana (Fungulieni)