Nyimbo Za Sifa
Wimbo 65 Mungu Msaada Wetu. Maneno ya wimbo
Mungu Msaada wetu
Tangu Miaka Yote
Ndiwe Tumaini letu
La zamani zote
Kivuli cha kiti chako
Ndiyo Ngome yetu
Watosha mkono wako
Ni ulinzi wetu
Kwanza havijakuwako
Nchi na milima
Ndiwe Mungu: chini yako
Twakaa salama
Na myaka elfu ni kama
Siku moja kwako-
Utatulinda daima
Tu wenyeji wako
Binadamu huondoka
Mwisho hana. kitu
Kama ndoto hutoweka
Ndiyo hali yetu
Ila Wewe Mungu wetu
Ndiwe wa kudumu
Ndiwe bora, Ngome yetu
Twakaa dawamu