Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 74 NIAMBIE, EE MLINZI nyimbo za wokovu
1
Niambie, Ee mlinzi,
Umepambazuka je!
Utukufu wa Zayuni;
Pana dalili zake?
Msafiri uondoke,
Utazame mbinguni,
Kiunoni ujifunge,
Ni kucha, alfajiri.
2
Mlinzi, inamulika
Nuru njiani mwako,
Dalili za kuja kwake,
Kwamba siku karibu;
Panda itakapolia
Itawaamsha wafu,
Watakatifu wa Mungu,
Kuwapa kutokufa.
3
Mlinzi, ione nuru
Ya mwaka wa Sabato;
Sauti zinatangaza
Ufalme ni karibu:
Msafiri ninaona
Mlima wa Zayuni,
Mji wa Yerusalemi
Nayo fahari yake.
4
Kwenye mji wa dhahabu
Anaketi Mfalme
Katika kiti kizuri:
Huku anatawala.
Pana amani po pote,
Mashamba husitawi;
Na ardhi ina rutuba;
Mito ni mitulivu.
5
Mlinzi, twakaribia
Nchi iliyo nzuri;
Twende mbele, tufurahi,
Nchi inachangamka.
Sikieni kuna wimbo
Wa waliookoka:
Kaza mwendo, Ujiunge
Na kundi kubwa hili.