Nyimbo za wokovu
Wimbo 186 Imbeni Juu Ya Pendo Maneno ya wimbo
Imbeni juu ya pendo la Yesu,
Na imbeni juu ya rehema;
Makao atufanyia,
Tumepewa neema.
Tuendapo mbinguni,
Itakuwa siku ya salama;
Tumwonapo Yesu,
Tutamshangilia Bwana.
Tukisafiri njiani mwetu,
Tutazikuta shaka nyingi;
Bali tukifika mwisho,
Hapo tutafurahi.
Tuwe waamini na wanyofu,
Na tumhudumu kila siku;
Tutamwona kwake mbingu,
Hiyo ni utukufu.
Twende mbele kupata zawadi,
Ni karibu kumwona Yesu;
Milango itafunguka Tuingiapo mbingu.