Nyimbo za wokovu
Wimbo 149 Mikononi Mwa Yesu Maneno ya wimbo
Mikononi mwa Yesu,
Kifuani mwake,
Mapenzi yanilinda
Sina hofu kamwe;
Ansha tuma wajumbe
Kuleta habari,
Ya kunifurahisha
Katika safari:
Mikononi mwa Yesu,
Kifuani mwake,
Mapenzi yanilinda Sina hofu kamwe.
Mikononi mwa Yesu,
Tashwishi sinayo;
Maonjo hayadhuru,
Madhambi yahamo.
Nikiwa na Mwokozi
Sioni majonzi;
Mashaka ni machache,
Machache machozi:
Yesu Mwokozi wangu
Akafa mtini:
Yesu, Mwamba wa kale
Namtumaini.
Namngojea Bwana,
Mchunga, Rafiki,
Hata kupambauka,
Huko mashariki.