Nyimbo za wokovu
Wimbo 84 Nimejazwa Na Furaha Maneno ya wimbo
Nimejazwa na furaha,
Tangu Roho akaja;
Hukaa nasi daima,
Moyoni mwa hakika.
Utulivu wa rohoni
Umekaa moyoni;
Roho wa Bwana aniletea
Utulivu moyoni.
Atuleteaye Uzima Ni Roho Mtakatifu;
Kutoamini aondoa,
Kuchoka ageuza.
Kama mvua inyeshavyo,
Kama jua angani;
Ndivyo tumepewa Roho,
Kutoka mbinguni.
Ni wokovu wa ajabu
Kumwona uso wake;
Makao makamilifu