Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 31 TANGU KUAMINI nyimbo za wokovu
1
Ninao wimbo mzuri,
Tangu kuamini;
Wa Mkombozi, Mfalme,
Tangu kuamini.
Tangu kuamini,
Jina lake ‘tasifu,’
Tangu kuamini,
Nitalisifu jina lake.
2
Kristo anitosha kweli,
Tangu kuamini,
Mapenzi yake napenda,
Tangu kuamini.
3
Ninalo shuhuda sawa,
Tangu kuamini,
Linalofukuza shaka,
Tangu kuamini.
4
Ninalo kao tayari,
Tangu kuamini;
Nililorithi kwa Yesu,
Tangu kuamini.