Nyimbo za wokovu
Wimbo 63 Piga Kelele Maneno ya wimbo
Piga kelele!
Adui yule,
Bendera shike
Kwa Bwana;
Vaa silaha
Mwenye Imara,
Litegemee Neno lake.
Zindukeni askari wa jeshi,
Enezeni neno la Mungu;
Twende Mbele, tuimeb
Kapitani ni Bwana Yesu.
Tuwe hodari
Tukisafiri,
Juu ya adui
Tushinde;
Silaha zetu
Zing`ae kwetu
Na tushinde
Tusianguke.
Mungu wa wote,
Kwa sisi sote.
Utusikie
Na neema;
Mwisho vitani
Kwa duniani
Tuvae taji
Mbele yako.