Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 184 PANAPO PENDO nyimbo za wokovu
1
Vitu vyote ni sawa,
Panapo pendo;
Kila sauti tamu,
Panapo pendo.
Pana amani pale,
Na furaha nyumbani,
Siku zote salama
Panapo pendo.
Panapo upendo –
Siku zote salama,
Panapo pendo
2
Furaha i nyumbani,
Panapo pendo;
Hapana machukizo,
Panapo pendo.
Chakula ni kitamu,
Mashamba yasitawi.
Maisha ni kamili,
Panapo pendo.
3
Hata mbinguni juu,
Pana furaha
Wakiona upendo
Nyumbani mwetu
Macho yanapendezwa
Na viumbe vya Mungu,
Naye Mungu huona,
Panapo pendo.
4
Ee Yesu niwe wako,
Wako kabisa,
Ndipo patakuwako
Pendo nyumbani;
Nitakaa salama,
Sitaifanya dhambi;
Nitabarikiwa tu
Panapo pendo.