Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 168 TARUMBETA YA MWANA nyimbo za wokovu
1
Tarumbeta ya Mwana
Itakapolia mara,
Milele itakapo pambazuka,
Nao wa haki watakapo
Kusanyika ng’ambo,
Majina yaitwapo lo niweko.
Majina yaitwapo, lo-
Majina yaitwapo, lo-
Majina yaitwapo, lo-
Majina yaitwapo, lo-niweko.
2
Siku ile watakatifu
Watakapoamka,
Na kuondoka huru kaburini,
Watakapokusanyika
Makaoni kule juu,
Majina yaitwapo lo niweko.
3
Tutende kazi kwa Yesu
Mchana kutwa kwa bidii,
Tutangaze kote
Pendo lake kuu,
Nayo kazi itakapotimika
Hapa chini,
Majina yaitwapo lo niweko.